Wednesday, July 20, 2011

Mahafali ya kuwaaga Wanafunzi wa kiislamu MNMA yanatarajia kufanyika tarehe 23/07/2011

Jumuiya ya Wanafunzi wa kiislamu MNMA inatarajia kufanya mafahali ya kuwaaga wanafunzi wa kiislamu wanaomaliza masomo yao katika ngazi ya cheti, stashahada na shahada siku ya jumamosi tareh 23 mwezi huu kuanzia muda wa saa 2 asubuhi hadi 10 jioni katika jengo la utamaduni.
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo anatarajiwa kuwa  Mkurungezi  wa taasisi ya kiislamu Munazamat al dawaa afrika mashariki  Dk Khalid Abdallah, pia Wageni wengine mbalimbali wanatarajiwa kufika kama Sheikh Baselehe, Ustadh Mohamedi Jalajala na Amiri wa amsya mkoa wa dar es salaam pamoja na Maamiri wa vyuo mbalimbali vya kiislamu.

No comments:

Post a Comment