Sunday, July 24, 2011

Waislamu wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wapata mfadhili wa kuwajengea Msikiti

Hatimaye kile kilio cha muda Mrefu cha Wanafunzi na Wafanyakazi wa kiislamu katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere juu ya kupata sehemu ya kufanyia ibada kimepatiwa ufumbuzi  baada ya  taasisi ya kiislamu ya Munazamati Al dawaa kutoa kauli ya kubeba jukumu hilo.

Kauli hiyo ambayo imetolewa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Afrika Mashariki Sheikh Salum Masoud katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kiislamu wanaomaliza masomo yao katika ngazi ya cheti, stashahada na shahada katika chuo hicho.

Sheikh Masoud ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alitoa kauli hiyo ya kubeba jukumu la ujenzi wa sehemu ya kufanyia ibada wakati akijibu risala iliyotolewa na wahitimu.

Pia Aliwataka Wanajumuiya ya kiislamu chuoni hapo kujenga mahusiano mazuri na taasisi yake na vyuo vingine ili waweze kuendeleza mbele harakati za uislamu katika chuo hicho, pamoja hilo alitoa vitabu  vya adabu katika uislamu kama zawadi yake kwa wahitimu.

Mbali na Mgeni huyo rasmi pia mahafali hayo yaliudhuriwa na Masheikh mbalimbali kama Sheikh Ally Baselehe, Mohamedi Jalala na Mkuu wa Masoko kitengo cha huduma za kibenki katika mfumo wa kiislamu Benki ya NBC Yasiir Salim ambapo walitoa mada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment