Saturday, November 26, 2011

WAISLAMU WATAKIWA KUTAFUTA ELIMU ITAKAYO MUONGOPA MWENYENZI MUNGU

Waislamu wametakiwa kutafuta elimu ambayo itakuwa na tija katika uislamu ili iweze kuwasaidia katika harakati, mapambano na kujitambua dhidi ya mifumo iliyopo ya kikafiri. Hayo yamesemwa na Sheikh Mohamed Jalala katika kongamano la kuwakaribisha wanafunzi wapya wa kiislamu katika chuo cha kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo kigamboni.

" Elimu ambayo itamfanya Muislamu aweze kuingamizi dunia kama Hiroshima na Nagasaki au kwenda kinyume na maamrisho ya Allah S.W basi ni batili na haifai" alisema Sheikh Jalala.

Pia Aliongezea kuwa Mwenyezi Mungu alimtaka Mtume Wetu Muhammadi S.A.W masomo yote lakini atambue kuwa hayo masomo lazima kwanza asome kwa ajili ya Mola wake. Kwa vile elimu nzuri itaijenga jamii katika mifumo ya kiuadirifu na nidhamu katika kujiletea maendeleo.

Naye Ustadh Mustapha Muhammadi ambaye ni Wafunafunzi wa Shahada ya Uzamifu ya uhandisi wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, aliwataka Waislamu waweze kutambua umuhimu wa kutumia wakati ipasvyo wakati wa kuendea masuala yao mbalimbali hususan masuala ya kielimu na katika ufanyaji wa ibada.

" Utunzaji mzuri wa wakati unatengeneza perfomance nzuri katika masomo na pia sio tu huko bali upelekea kufanya ibada ambazo zimekamilika kwani kila ibada imewekewa muda maalum Swala, Funga na hata Hija " alisema Ustadh Muhammadi.

Pia alisema kila kitu alichanacho muislamu kina umuhimu wake katika matendo yaliyobora, hivyo aliwataka Wanafunzi wa kiislamu hapo chuo kutambua kuwa nafasi waliokuwa nayo ya kusoma ni muhimu na waitumia ipasavyo ili iwezeleta faida katika uislamu kiujumla.

Ustadh Mustapha Muhammadi akiwasilisha mada.


Naibu Amiri wa Jumuiya Hassani  Daudi, Amiri wa Jumuiya Mhini Mganga na Amiri wa Daawa Khamis Hamad  wakiishikiliza kwa makini moja ya mada zilizokuwa zikiwakilishwa.


 Katibu Msaidizi wa TAMPRO (Taasisi ya Wanataalum wa kiislamu Tanzania) Haji Mrisho akitoa Mada katika kongamano.


                        Amiri wa Jumuiya Muhini Mganga na Sheikh Jalala wakisikiliza mada kwa makini.


  Amiri wa TAMSYA taifa Jafar Saidi Mneke na Naibu Amiri wa MSAM Hassani Daudi.

                                              Baadhi ya  Wanafunzi waliodhuria kongamano.

                                Wanafunzi wakisikiliza kwa makinia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.


 

No comments:

Post a Comment