Tuesday, November 27, 2012

Sherehe ya kuwakaribisha Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na harambee ya ujenzi wa msikiti

Mkurugenzi wa Islamic Foundation Sheikh Arif Mbarak Nahd ambaye alikuwa mgeni rasmi wa sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Sheikh Nahd ameahidi kujenga msikiti katika eneo ambalo jumuiya hiyo imepewa na uongozi wa chuo kwa ajili ya kujenga nyumbani hiyo ya ibada.
Msomaji wa risala Salum Kilingo akiisoma risala iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa Mgeni rasmi Sheikh Arif Mbarak Nahd Mkurugenzi wa Taasis ya Islamic Foundation katika siku hiyo ya sherehe ya kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza



Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi wa NSSF DK Ramadhani Dau akitoa moja ya mada zilizowasilishwa katika Sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza na harambee ya ujenzi wa msikiti katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu ya Nyerere. Dau alisisitiza kujiamini kwa Wanafunzi wa Kiislamu ili kuweza kukabilia na changamoto mbalimbali pindi wawapo chuoni na makazini.Pia Dk Dau alihaidi kutoa kiasi cha Shiling milion Kumi na kompyuta pakato na machine ya photocopy kwa Jumuiya hiyo.

Viongozi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Mazinge.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakisikiliza moja ya mada zilizokuwa zinawasilishwa kwa makini.


 

No comments:

Post a Comment