Tuesday, November 27, 2012

Sherehe ya kuwakaribisha Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na harambee ya ujenzi wa msikiti

Mkurugenzi wa Islamic Foundation Sheikh Arif Mbarak Nahd ambaye alikuwa mgeni rasmi wa sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Sheikh Nahd ameahidi kujenga msikiti katika eneo ambalo jumuiya hiyo imepewa na uongozi wa chuo kwa ajili ya kujenga nyumbani hiyo ya ibada.
Msomaji wa risala Salum Kilingo akiisoma risala iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa Mgeni rasmi Sheikh Arif Mbarak Nahd Mkurugenzi wa Taasis ya Islamic Foundation katika siku hiyo ya sherehe ya kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza



Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi wa NSSF DK Ramadhani Dau akitoa moja ya mada zilizowasilishwa katika Sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza na harambee ya ujenzi wa msikiti katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu ya Nyerere. Dau alisisitiza kujiamini kwa Wanafunzi wa Kiislamu ili kuweza kukabilia na changamoto mbalimbali pindi wawapo chuoni na makazini.Pia Dk Dau alihaidi kutoa kiasi cha Shiling milion Kumi na kompyuta pakato na machine ya photocopy kwa Jumuiya hiyo.

Viongozi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Mazinge.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakisikiliza moja ya mada zilizokuwa zinawasilishwa kwa makini.


 

Saturday, November 26, 2011

WAISLAMU WATAKIWA KUTAFUTA ELIMU ITAKAYO MUONGOPA MWENYENZI MUNGU

Waislamu wametakiwa kutafuta elimu ambayo itakuwa na tija katika uislamu ili iweze kuwasaidia katika harakati, mapambano na kujitambua dhidi ya mifumo iliyopo ya kikafiri. Hayo yamesemwa na Sheikh Mohamed Jalala katika kongamano la kuwakaribisha wanafunzi wapya wa kiislamu katika chuo cha kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo kigamboni.

" Elimu ambayo itamfanya Muislamu aweze kuingamizi dunia kama Hiroshima na Nagasaki au kwenda kinyume na maamrisho ya Allah S.W basi ni batili na haifai" alisema Sheikh Jalala.

Pia Aliongezea kuwa Mwenyezi Mungu alimtaka Mtume Wetu Muhammadi S.A.W masomo yote lakini atambue kuwa hayo masomo lazima kwanza asome kwa ajili ya Mola wake. Kwa vile elimu nzuri itaijenga jamii katika mifumo ya kiuadirifu na nidhamu katika kujiletea maendeleo.

Naye Ustadh Mustapha Muhammadi ambaye ni Wafunafunzi wa Shahada ya Uzamifu ya uhandisi wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, aliwataka Waislamu waweze kutambua umuhimu wa kutumia wakati ipasvyo wakati wa kuendea masuala yao mbalimbali hususan masuala ya kielimu na katika ufanyaji wa ibada.

" Utunzaji mzuri wa wakati unatengeneza perfomance nzuri katika masomo na pia sio tu huko bali upelekea kufanya ibada ambazo zimekamilika kwani kila ibada imewekewa muda maalum Swala, Funga na hata Hija " alisema Ustadh Muhammadi.

Pia alisema kila kitu alichanacho muislamu kina umuhimu wake katika matendo yaliyobora, hivyo aliwataka Wanafunzi wa kiislamu hapo chuo kutambua kuwa nafasi waliokuwa nayo ya kusoma ni muhimu na waitumia ipasavyo ili iwezeleta faida katika uislamu kiujumla.

Ustadh Mustapha Muhammadi akiwasilisha mada.


Naibu Amiri wa Jumuiya Hassani  Daudi, Amiri wa Jumuiya Mhini Mganga na Amiri wa Daawa Khamis Hamad  wakiishikiliza kwa makini moja ya mada zilizokuwa zikiwakilishwa.


 Katibu Msaidizi wa TAMPRO (Taasisi ya Wanataalum wa kiislamu Tanzania) Haji Mrisho akitoa Mada katika kongamano.


                        Amiri wa Jumuiya Muhini Mganga na Sheikh Jalala wakisikiliza mada kwa makini.


  Amiri wa TAMSYA taifa Jafar Saidi Mneke na Naibu Amiri wa MSAM Hassani Daudi.

                                              Baadhi ya  Wanafunzi waliodhuria kongamano.

                                Wanafunzi wakisikiliza kwa makinia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.


 

Thursday, August 18, 2011

                               RAMADHAN KARIM

Matukio ya Sherehe ya Mahafali katika Picha

Meja wa Masoko wa Benki ya NBC katika kitengo kichohusika na Benki ya kiislamu Zahir Salim akitoa mada ya kutumia mfumo wa kibenki wa kiislamu.

Baadhi ya Wahitimu wakisikiliza kwa Makini mada zilizokuwa zikitolewa,

Naibu katibu wa Jumuiya ya Kiislamu MNMA Salum kilingo na Mweka hazina wa Jumuiya hiyo Sada Haji Wakasi wakijadili jambo nje ya ukumbi wa jengo la utamaduni ambapo mahafali yalifanyika.

Baadhi  ya Wahitimu na Wageni wakipata Chakula

Amiri wa Tamsya Mkoa wa Dar es Salaam na Katibu wa Jumuiya Selemani Msuya wakisiliza kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa.
Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya kuwaaga Wahitimu wa Kiislamu Chuo cha Kumbukumbu ya Mawlimu Nyerere. Mahafali hayo yaliandaliwa na Jumuiya wa Waislamu Chuo hapo.

Kutoka kushoto ni Doto Ramadhani kutoka Benki ya NBC kitengo cha huduma za kibenki za kiislamu, Amiri wa Dawa Jumuiya ya Kiislamu MNMA, Afisa Habari wa Jumuiya Mbaruku Mchopanga na Amiri wa Jumuiya Mganga Muhidini.
Kutoka kushoto ni Amiri wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu MNMA Sheikh Mganga Muhidini akipata chakula na Meneja Masoko Benki ya NBC kitengo cha benki ya kiislamu Zahir Salim (katikati) na Sheikh Ally Baselehe. 

Sunday, July 24, 2011

                     Sheikh Mohamedi Jalala akitoa mada ya Vijana na Utandawazi katika mahafali hayo.